Thursday, July 12, 2012

Vijana ina maana ya "youth".

Sisi ni wanachama vijana wa Youth Challenge International (YCI), Zanzibar.

Haya ni mawazo yetu.


- -

Vijana means "youth".

We are the youth members of Youth Challenge International (YCI), in Zanzibar. 

These are our thoughts. 


"Vijana Tuamkeni" ("Oh Youth, Wake Up")

[Kiswahili]

Bismillahi naanza kwa jina lake muweza
Mola mwenye miujiza hakuna anomuweza
Lotutoa kwenye giza mwangani akatukweza
Kwani yeye ndo wa kwanza wa  kupewa shukurani

Pili nakushukuruni nyote humu mlo ndani
Yenu kutia kapuni mkaja humu darasani
Tena mkawa makini mkwa hamuvutani
Kubwa hilo letu lengo Elimu kukufikisheni

Elimu kufikisheni lengo letu ndilo hilo
Madawa tuyaepukeni hala tena mbiombio
Malengo tuyafikeni kupita matarajio
Vijana tuamkeni madwa hayana mana

Madawa hayana mana vyema tukayaachana
Tena tukashikamina hasahasa si vijana
Ukweli kuambiana bila hata kufichana
Vijana tuamkeni madawa hayana mana

Tabia tuzibadili tuepuke na dhihaka
Wengi wamekwenda hri ni madada na makaka
Hwajui zao hali kujiona waubuka
Vijana tuamkeni tabia tuzibadili
Mwisho ninamalizia kwa pongezi kuzitoa
Kwa wana polisi jamia ukumbi kutugaia
Na kuonesha yao nia vijana kuwagomboa
Hasa wao viongozi walofanya kubwa kazi

Pia na wetu walimu walio wataalamu
Kutupatia elimu sio chungu tena tamu
Tene ilio muhimu kwa kilia mwanadamu
Jamani nasisitiza madawa tuyawacheni

- - 

[English] 
 
To begin with the name of Allah, the Almighty
Oh, a miracle, no one can do such a thing like He can
The One who takes away the dark sky and elevates us
Has He given us the membrane of the first gratitude.

Second I appreciate all the foods in this country
You put us in this class, to come and listen to us
Again, you were careful and cooperative
Great was our goal to send you education.

Education, to share, that is our goal
We should stay away from drugs, immediately
Goals beyond expectations must be reached
Oh Youth, wake up! Drugs are meaningless, stay away.

Drugs do not mean well, we must stay away
Again we must work together, especially the young youth
Facts speak loudly, we must not keep it secret
Oh Youth, wake up, drugs are meaningless, stay away.

We have to change and avoid the ridiculous behavior
Many have gone crazy, dear sisters and brothers
Their condition, they don’t know, they feel crushed
Oh Youth, we must change, drugs are meaningless, stay away

Finally I end with a compliment to give
To have the society police and assist one another
And to show our youth freedom and liberate them
Especially their leaders, encourage them to do great work.

Also with our expert teachers
Give us the sweet education, not the bitter
To give us this education is something important for mankind
Oh Society, I insist that we stay away from drugs. 

- - 

 PRESENTED BY:

1 OMAR MOH’D BAKAR
YCI Vijana - July 2012. 
2